Ad Code

Responsive Advertisement

Mabasi mawili yagongana kisha yaingia korongoni, majeruhi wakimbizwa hospitalini Kutoka mbeya kwenda tunduma

  

Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri katika Mabasi mawili tofauti kutoka Mbeya kwenda Tunduma wamejeruhiwa katika ajali ya Barabarani eneo la mlima Iwambi Barabara Kuu ya TANZAM majira ya saa mbili usiku.

Baadhi ya mashuhuda wamedai chanzo cha ajali ni mwendokasi na uzembe wa moja ya Mabasi hayo kujaribu kulipita basi jingine ndipo lilipopoteza mwelekeo kisha kuligonga basi jingine na yote yaliingia korongoni.

Taarifa za awali kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei eneo la ajali hakuna kifo chochote kilichotokea na idadi ya majeruhi bado haijafamika na ameelekea hospitali teule ya Ifisi ili kujua madhira ya abiria. Ulinzi umeimarishwa eneo la ajali chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi Debora Lukololo.


Post a Comment

0 Comments

Ad Code

Responsive Advertisement