First Lady huyu amesema kuwa mashambulizi siku hiyo yalianza usiku wa saa saba ndipo walianza sikia risasi zinapigwa kwenye chumba chao na wakaamua kujificha lakini Watu hao hawakuishia hapo kwani waliingia mpaka ndani ya nyumba na kuvunja mlango na kuingia mpaka chumbani kwao.
Anasema wale Wauaji walikuwa wametumwa kwani walivyovunja chumba chao walikuwa na kazi moja tu ya kutafuta nyaraka na walipozipata wakapiga simu na kuwaambia waliowatuma kuwa wameshazipata na kisha kumsogelea Rais na kupokea maelekezo ambayo yaliashiria kuwa ndie Mtu sahihi anaetakiwa kuuwawa.
Mpaka wakati huo tayari Rais na Mke wake walikua wameshajeruhiwa kwa risasi nyingi na Wauaji hao wakapewa agizo kuwa wamalizie kumuua Rais Jovenel Moise “hatukujua kama wangefanikiwa kufika kwenye chumba tulikojificha maana nje tulikua na Walinzi 30 au 50″- Martine Moise

0 Comments